Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Moto waendelea kuwaka Nyumba ya maajabu Ugombolwa Tabata


Huko Tabata Mtaa wa Ugombolwa kuna nyumba maarufu kama nyumba ya maajabu kutokana na vituko mbalimbali vilivyowatokea wapangaji wake kiasi cha kufanya wapangaji hao kukimbia huku wale walioshindwa kutafuta hifadhi mara moja wakiweka vyombo vyao katika kituo kidogo cha Polisi mtaani hapo Ugombolwa.Pichani ni sehemu ya mbele ya nyumba hiyo ambayo kwa sasa haina mpangaji yeyote.Siku ya Jumatatu tarehe 7/5 walialika wana maombi ambao walishusha neno ili kukemea mauzauza hayo ya moto kuwaka na kupakwa kinyesi cha binadamu ukutani bila kufahamu anae paka ni nani walipoanza ukawaka moto mkubwa tena kwenye kilekile chumba alichokuwa anatumia mjukuu wa mwenye nyumba.Hivyo baadhi ya wanamaombi na baadhi ya watu wakakimbia kuogopa moto huo.

Dirisha hili ndilo humo chumbani moto huwaka mara kwa mara liko upande wa barabara ambapo wapita njia mara nyingi hushuhudia mauzauza hayo ya kuwaka moto.Hata kwa kuangalia hapo unaona katika taswira dirisha hilo likiwa jeusi kutokana na moto huo wa mara kwa mara.Vituko vya nyumba hiyo ni pamoja na wapangaji enzo hizo kukuta ugali wa moto chooni bila kujua alieweka ni nani,kurushwa kwa mawe juu ya bati usiku na kupakwa kwa kinyesi kwenye kuta.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top