Loading...
Nje ya uwanja.
Hizi ni jezi za Yanga ambazo zilikuwa zinauzwa jana kabla mpambano wao na watani Simba.Jezi kama hizi hazijulikani kama zinazifaidisha timu kimapato au ni wajanja wacache walio amua kutengeneza jezi hizo na pesa kuishia kusiko julikana.
Hapo ni katika geti la kuingilia ndani ya uwanja wa Taifa mashabiki wakiwa tayari kuingia kushudia mtanange huo.
Pia mabingwa wa mijadala nao hawakukosekana vikundi kama hivi vilikuwa na wazungumzaji wakuu ambao walikuwa wakimwaga data mbalimbali na wengine wakiwa kimya kuwasikiliza ilimradi muda uende mpambano uanze.
Wajasiria mali nao hawakukosekana kila kona wakitoa huduma zote muhimu za mlo wa mchana kwa wale waliowahi mpambano huo ili wapate nguvu za kutosha kushangilia dakika zote 90.
Wengine waliona isiwe tabu nitausikilizia hapahapa nje Jamaa akiwa na redio yake isiyo banduka masikioni akisubiria mpambano huo wa watani wa Jadi.Mpambano huo uliishia kwa Simba kubanjua Watani zao Yanga goli 5 kwa nunge.
Post a Comment
CodeNirvana