Loading...
Sami Hyypia aula Bayer Leverkusen
Sami Hyypia, May 2005
Mchezaji wa zamani wa Liverpool,Sami Hyypia alieichezea Anfield kati ya 1999 na 2009,amethibitishwa rasmi kuwa Kocha MKuu wa Bayer Leverkusen baada ya kuwa Kocha wa muda toka mwanzoni wa April alipofukuzwa Kocha Robin Dutt baada ya timu hiyo kusuasua katika Ligi nchini humo.
Akiwa ameiongoza timu hiyo kwenye michezo sita akiwa kashinda 4 na kutoa droo 2 na kufanikiwa kuipeleka timu hiyo kwenye Michezo ya Ligi ya Europa Beki huyo mwenye miaka 38 sasa atasaidiana na Sascha Lewandowski,na amepewa mkataba wa miaka 3 hapo BayArena.
Hyypia, ambae ameichezea Anfield mechi 464 katika kukaa kwake Klabuni hapo amefurahishwa na Uongongozi wa Bayer kumpa mkataba huo.
2 maoni
Mkuu naona mabadiliko bado yanaendelea.Background colour bado haijatulia.
ReplyMkuu tunalihangaikia hilo mkuu ili walaji mpate kile mnachokihitaji Mkuu.Ukiwa na mapicha ,mashairi,ngonjera usisite kutuma chedichas@gmail.com
Reply