Loading...
Taswira ndani ya Uwanja wa Taifa
Ndani ya Uwanja hali ilianza kwa mashabiki kuanza kukaa kwenye majukwaa kama taswira inavyoonyesha hapo mashabiki wa Simba wakianza kuja kwa wingi kama inavyoonekana.
Uwanja ukiwa tayari kwa mechi hiyo ya wataniwa jadi ukionekana msano kabisa kwa mikiki mikiki hiyo ambapo iliishia kwa Simba 5-0 Yanga.
Vibweka navyo havikukosekana hapo washabiki wa Simba wakimuangalia shabiki wa Yanga aliokolewa na askari Polisi alipokuwa akipita upande wa Simba(Askari anaonekana akiwa kamziba shabiki huyo)
Nyomi ikiwa imesheheni tayari kwa mpambano huo wa watani wa jadi.
Mpambano wa watani wa jadi uliokuwa wa kukamilisha ratiba ambapo watani hao walikuwa wakipambana na kuishia kwa SIMBA 5-0 YANGA na kunogesha sherehe ya kukabidhiwa simba ubingwa wao ambao waliunogesha vilivyo.
Post a Comment
CodeNirvana