Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Taswira za Ubungo


Eneo la Ubungo ambalo lilifanyika zoezi la kuwahamisha wafanyabiashara ndogondogo''machinga'' hivyo eneo hilo kuonekana likiwa safi na kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano uliokuwepo mwanzo.Pichani ikionekana sasa magari yakiwa yamepaki hovyo na pikipiki pia huku wapiga debe nao wakipata kahawa kwa mbaali baada ya kazi nzito ya kuita wateja.

Taswira ndani ya kituo cha daladala kikionekana kwa nafasi nzuri kuliko hapo mwanzo ambapo kulikuwa na idadi kubwa ya wajasiria mali ambao walilfanya eneo hilo kupitika kwa tabu sana kwa wasafiri wanaotumia daldala kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji na kuleta taswira isiyopendeza.
Mbele ya ofisi za MAkao Makuu ya TANESCO taswira ikiwa ya kuvutia baada ile kadhia ya machinga kuondolewa na hivyo kufanya eneo hilo kuwa safi na hata wapanda baiskeli wakiweza tumia vyombo vyao hivyo.


Taswira zikizidi tanabaisha jinsi zoezi hilo lilivyofanikiwa kwa muonekano huo na zilichukuliwa kipindi ambapo huko nyuma kabla ya zoezi mida hiyo walikuwa tayari wameshafunga njia kwa kutandaza bidhaa zao chini.


Lakini kuna mchoma mahindi mabichi yeye ameendelea kukomaa hapo akiwa yupo kwenye kituo cha daladala ziendazo Kimara,Mbezi karibu na makao Makuu ya TANESCO hapo anaonekana akimuuzia mteja(jina kapuni) wake ambae nae anaonekana akimtania Mzee huyo (jina halikuweza kupatikana) kuwa mgambo hao wanakuja kiasi kilichomfanya Mzee huyo kutaharuki lakini mwishowe ilikuwa utani na akaendeleza libeneke kama kawa.





author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

2 maoni

Hayo maindi ya kuchoma mie fulu kutamani yani!

Reply

mkuu unakaribishwa sana kupata Hindi japo moja

Reply
CodeNirvana
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top