Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Hapa na pale Buguruni


Hapa ni Shell Buguruni ukiwa umeshuka kama watokea Ubungo/Tabata unaelekea maeneo ya Sokoni Buguruni

Watu wakiwa kwenye mikiki mikiki kuwahi sokoni wengine wakiwa waenda panda gari kuelekea maeneo tofauti hapa ni ukiwa umetoka Shell Buguruni ukikaroobia kituo cha Muhimbili/Kivukoni hapo Buguruni.

Kamera yetu ikiwa katikati ya barabara kuelekea Sokoni Buguruni na ukiwa unakiona kituo pamoja na soko la buguruni kwa mbaali hapo


Hapo ni Sokoni Buguruni wasafiri wakisubiri usafiri kuelekea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam hapo watu 'nyomi' gari likitokea mwenye ubavu ndie anapata kiti cha kukalia wengine huwahi kwa kupitia madirishani Tembelea kijiweni kila wakati tukiwapata wale warukao madirisha tutawaletea hapa hapa bila kusita.

Kila mmoja akiangalia gari linaloingia linaelekea eneo analotaka kwenda au sio ili aweze wahi kupanda hapa ni Buguruni Sokoni

Bi dada huyu nae akihangaika na mzigo wake baada ya kufanya manunuzi sokoni hapo ili nae akauze mtaani kwenye Genge lake. Sehemu hiyo imekuwa na adha ya usafiri mida ya asubuhi pale idadi kubwa ya watu wakienda maeneo mbalimbali ya jiji ,Kawe,Msasani ,Masaki na Mwananyamala.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top