Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Tunakuletea Hotuba fupi ya Mh.John Mnyika akitoa neno la Shukrani hii ni kupitia ukurasa wa Twitter.



anatoa hotuba kwa wananchi!

"Tunawashukuru sana kwa sala na swala zenu.Pamoja na mifumo dhaifu ya kimahakama tumepata ushindi''

"Hii ni ishara na salamu ya mwaka 2015"

"Alishutumiwa kwa ufisadi,akafungua shtaka leo mahakama imetenda stahiki"

"Aliyenifungulia kesi aliwahi kukamatwa na Takukuru.Nataka Takukuru iseme nini hatma ya kesi yake ya rushwa"

"Ni nyakati ambazo tunashuhudia chama tawala,CCM kikiwa kinashindwa vibaya hata kulia hadharani"

"Jitihada hizi zinatoa haja zaidi na zaidi kuhakikisha tunapata katiba mpya iliyo nzuri sana"

"Ndugu zangu,huu ni ushindi wa watu.Si wangu peke yangu"!


"Namshukuru MUNGU amemuongoza vizuri Jaji,kukataa uongo,ufisadi na upotoshaji.Amekiri mashtaka hayakuwa na msingi"


"Imedhihirisha umakini,uwajibikaji,uaminifu"

"Wingi wenu huu,na salamu za kheri ktk mitandao inadhihirisha sana imani yenu kwangu.Nitawatumikia!"

"Toka mwaka 2010 kesi imekuwa ikinipotezea muda wa kuwatumikia kikamilifu wananchi!

"Nawaahidi kuendelea kusimamia haki,na kuwatumikia kwa uadilifu sana"

"Tuliwashinda uwanjani wakakimbilia mezani,nako tumewashinda"

Hukumu imetoka ktk hali ambayo nchi ipo ktk hali mbaya,gharama za maisha zimepanda mno!"

Tutashughulika na maji,uwajibikaji,elimu nk lakini tusisahau KATIBA!26th Mei,jumamosi hii tukutane Jangwani!"

Waniongezea muda wa kuhakikisha mziki unaeleweka bungeni.Hakuna kulala!

"Mfikishie Rais,ile taarifa tuliyoikomalia Bungeni.Bado,tutaenda kukomaa zaidi na zaidi

"Tunahitaji uwakilishi unaotokana na watu.Na kuhakikisha tunauheshimu uwakilishi hu0''

"Busara za wazee ndiyo chachu ya ushindi,huku Vijana wakiwa nguvu ya Ushindi wetu

"Nikiwaambia tuingie barabarani,tuingie mpaka kieleweke

"Juzi nilimfikishia salamu waziri mpya wa Maji,na wa Nishati na Madini.Watende kazi niliyowaambia.Tutakutana Dodoma

"Daima nitaendelea kushukuru sana kwa sala na swala zenu.Tuendelee kuombeana

"Ni jambo gumu sana kufanya kazi ktk mifumo iliyooza kama hii

"Tarehe 21st Aug,2012 tutakuwa na harambee kubwa kusaidia elimu jimboni tuhakikishe tunakusanya zaidi ya 100Mil"

"Kura yangu ni 1 tu ktk kura elfu60+!Tufurahie pamoja wote.


KWA HISANI KUBWA YA Michael J.Dalali kupitia Ukurasa wake wa Twitter. ‏@MichaelDalali #UshindiMnyika
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top