Saturday, 05 May 2012 10:27
Fidelis Butahe
BAADA ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza lake la mawaziri ikiwa ni pamoja na kuwaondoa mawaziri sita waliokuwa wakishinikizwa wajiuzulu, wasomi wamesema kuwa kinachotakiwa kubadilishwa ni mfumo wa utawala na siyo sura mpya za mawaziri.
Wasomi hao waliozungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya Rais Kikwete kufanya uteuzi huo walisema mfumo ndio unaosababisha mambo kutokwenda sawa katika wizara na idara mbalimbali za serikali.
Mawaziri walioondolewa ni pamoja na Ezekiel Maige wa Maliasili na Utalii, William Ngeleja wa Nishati na Madini, Omar Nundu wa Uchukuzi, Cyril Chami wa Viwanda na Biashara, Hadji Mponda wa Afya na Ustawi wa Jamii na Mustafa Mkulo wa Fedha.
Mawaziri walionusurika katika sakata hilo ambapo pia walikuwa kashfa ni wawili, George Mkuchika na Jumanne Maghembe ambao hata hivyo wamehamishwa kwenye wizara zao za awali; Tamisemi na Kilimo. Akizungumza na Mwananchi akiwa nchini Ureno Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Emmanuel Mallya alisema licha ya kuwa mabadiliko yamefanyika lakini sio suluhisho kutokana na nchi kuwa na mfumo mbovu wa utawala.
Alisema mawaziri waliokumbwa na kashfa mbalimbali walitakiwa kusimamishwa kazi ili wachunguzwe na kama ingebainika hawana hatia wangerudishwa kazini. “Kama wangekutwa na hatia wangefunguliwa mashitaka, hii ingewafanya wengine kuogopa kutafuna mali za umma kwa kuhofia kuwa watasimamishwa kazi na kuchunguzwa” alisema Mallya. Alifafanua kwamba kitendo cha baadhi ya viongozi kuteuliwa si kizuri na kusisitiza kuwa inatakiwa liwapo baraza maalum la kuwafanyia usaili watu wanaofanya kazi za kuwatumikia wananchi na kuwatolea mfano Majaji.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alimpongeza Rais Kikwete kwa kufanya uteuzi huo ikiwa ni pamoja na kuwang’ oa mawaziri waliokuwa wakilalamikiwa, lakini alionyesha wasiwasi wake katika suala zima la mfumo wa uongozi na kusema kuwa ndio unaowafanya wananchi kulalamika kila kukicha.
“Rais amekidhi matakwa ya wabunge, wananchi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kuwaondoa mawaziri waliokuwa wakilalamikiwa, uamuzi huo unatosha na unaonyesha usikivu wake” alisema Dk Bana. Hata hivyo, Dk Bana alisema kubadilisha sura za mawaziri sio dawa na kwamba dawa ni kubadilisha mfumo mzima wa utawala.
“Kitendo cha waliokuwa manaibu waziri kupandishwa kuwa mawaziri ni jambo zuri, binafsi nadhani manaibu mawaziri wamekuwa wengi, angeweza kuwapunguza na utendaji wa kazi ungeendelea kuwa safi” alisema Dk Bana. Profesa mwingine wa chuo hicho, Gaudence Mpangala alisema mawaziri hao walitakiwa kujiuzulu baada ya ripoti ya CAG na ripoti za Kamati za kudumu za bunge kuanika kashfa zinazowakabili.
“Ilinishangaza kuona wengine wakijitetea wakati ripoti zilikuwa zinaeleza kila kitu, mtu ukiwajibika sio lazima uwe umetenda kosa, mbona Rais Ali Hassan Mwinyi aliwajibika kwa makosa ya wengine na baadaye akawa rais wa Tanzania,” alisema Mpangala.
Hata hivyo, Profesa Mpangala alisema kuwa tatizo sio kubadili baraza la mawaziri, kubadili mfumo mzima wa utawala na kusema kuwa uteuzi huo sasa unaonyesha wazi kuwa utamaduni wa kulindana ndani ya CCM unafika
Habari na Gazeti la MWananchi.
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana