Loading...
Kuelekea kusomwa Bajeti Dodoma vunja mbavu na Bajeti ya Mlalahoi Masanjawani
#BajetiyaMlalahoi Vocha ya jero iuzwe mia nne hamsini, ati listi tubaki na hamsini ya kuskrachi!
#BajetiyaMlalahoi Kile kishimo katika donati kitolewe, kinakula tu nafasi!
#BajetiyaMlalahoi Pakingi tauni ishuke, si tunapaki eti awa ouni riski ama?
#BajetiyaMlalahoi Safari za kwenda Bondeni kwa Madiba zishuke bei, bondeni, si ndege inashuka tu, unaweka frii!
#BajetiyaMlalahoi Ili sirikali ijipange na suala la ajira, inabidi ianze kumlipa kila mtu anayemaliza masomo halafu akakosa ajira!
#BajetiyaMlalahoi Sinza yoooote iwe na kodi moja ya nyumba! Si inakuwa ngumu kuelewa tofauti! Banda la uani laki, la pembeni laki mbili!
#BajetiyaMlalahoi Supamaketi wawe wanauza slesi za mikate. Kwani kila mtu ana uwezo wa kununua mkate mzima?!
#BajetiyaMlalahoi John Walker afike mwisho wa safari yake ili bei ya ile Whiskey yake ishuke. Muda wooote anatembea!
#BajetiyaMlalahoi MPs wote wawe wanapanda treni kutoka Dar kwenda Dodoma. Mwakye kaonyesha njia! Wakubwa zaidi treni fasti klasi!
#BajetiyaMlalahoi Gongo ihalalishwe rasmi, iitwe Whiskey ya Mlalahoi, Made In Tanzania.
#BajetiyaMlalahoi Tufikirie na suala la posho ya mapoudaaaa kwa wanasihasa, ili politiksi iache kuitwa showbiz for ugly people!
#BajetiyaMlalahoi #Budgetyamasufferer Logo ya apple ing'atwe tena kusudi bidhaa za apple zishuke bei!
#BajetiyaMlalahoi Kama Ice Cream ni buku jero, ifike pahala tumwambie muuzaje ailambe hadi ibaki ya buku ndo atuuzie!
#BajetiYaMlalaho Unga wa Sembe wa Baharesa uwekewe fleva ya kuku, ati listi ukila ugali kwa mchicha, ugali uwe una kasimeli ka kuku
#BajetiYaMlalahoi Siku ya kwenda kutoa mahari, uwe unaruhusiwa kutoa risiti za matumizi ulifanya kwa binti wakati mko uchumba! Zijumlishiwe!
#BajetiYaMlalaho #Budgetyamasufferer Watu wenye vishilingi kichwani pia walipe kodi!
#BajetiYaMlalahoi Pakingi fii iruhusiwe malipo mbadala, hata lifti kwa wale wanachukua hela ya pakingi!
#BajetiYaMlalahoi Hivi Wabonge hawawezi kutumia Vitz ama ni gani?
#BajetiYaMlalahoi Hivi hawawezi kuweka sheria hiki chakula kinaitwa Pizza kikauzwa kwa vipande? Nzima imekuwa bei juu sana!
#BajetiYaMlalahoi Kuwe na kaplani kakufanya Masaki nzima iwe hostelzi za wanafunzi! Itapandisha morali ya kufaulu!
#BajetiYaMlalahoi #BudgetYaMasufferer Na bei ya mahindi ya kuchoma ishuke! Kwani inatumika gesi kuchoma mahindi ama ni gani?!
#BajetiYaMlalahoi #BudgetYaMasufferer Hii "Road To Success" ijengwe na Wachina ili ikamilike fasta na jam iishe!
#BajetiYaMlalahoi Hii reli ya kati hamuwezi kutanua ikafika kwa Madiba? Watu wameteseka mno na kuzamia meli!
#BajetiYaMlalahoi Fonti saizi ya magazeti iongezwe hadi 70 ili tusome vizuri tukiwa kwenye daladala. Pipo 6 gazeti moja!
#BajetiYaMlalahoi Ipitishwe sheria kuzuia kujibu nyimbo za bongo fleva. Saidia kukuza kipaji cha Inspekta, msaidie asijibu nyimbo!
Masanja Mkandamizaji @masanjawani
#BajetiYaMlalahoi BodaBoda ziwekewe ngao kabisa. Kwani hamuoni ni hatari mtu anachomekea lori la mchanga bila ngao wala helmenti!
Soma zaidi kwa kumfutilia huko twetter kwa kupitia.......
Masanja Mkandamizaji @masanjawani
Post a Comment
CodeNirvana