Loading...
Home
» Kutoka Facebook
» Kwenye Facebook yake:Nape aeleza kuhusiana na yaliyojiri Bungeni Leo kuhusiana na Hali ya Uchumi
Kwenye Facebook yake:Nape aeleza kuhusiana na yaliyojiri Bungeni Leo kuhusiana na Hali ya Uchumi
Nilikuwa nikisikiliza Bunge na kusikia hotuba juu ya hali ya uchumi hapa nchini na nikajiuliza hivi hawa "watani" wetu wanaopita kuchangisha watu nchi nzima na kunadi kuwa hali yetu ya kiuchumi ni "mbaya sana" na wengine wakaandika makala kwenye magazeti kuwa serikali haina hata uwezo wa kuagiza mahitaji ya mwezi nje ya nchi na HAZINA imekauka..,nilijiuliza kuwa hayo wameyatoa wapi..? ni uvivu wa kufuatilia na kusoma ripoti za serikali juu ya hali ya uchumi au ni dhamira ya kukusudia kupotosha na kudanganya umma wa watanzania..,
Nimekuwa nikisoma na kufuatilia ripoti na taarifa mbalimbali za uchumi za nchi mbalimbali duniani na kufarijika baada ya kugundua kuwa hali yetu ya kiuchumi inaelekea vizuri kuliko nchi nyingi hata zile zinazotajwa kuwa zilizoendelea za kule Ulaya na Asia.
Mathalani kwa India, takwimu za uchumi zinaonyesha kuwa GDP imeendelea kushuka kwa 5% tangu mwaka 2010.,according to economic watch.,Ugiriki wamekuwa wakitapatapa kujinasua kwenye madeni makubwa waliyonayo,lakini pia wanayo hatari kubwa katika kupungukiwa nishati ya umeme ambayo ni msingi katika shughuli za uzalishaji nchini humo hata serikali kulazimika kutumia dola milioni 50 za dharura kutoka hazina yao kukabiliana na hatari hiyo. Na hii ni nchi yenye watu wasiozidi milioni 11.5.
Pia, Benki ya dunia imeonesha wasiwasi wake juu ya hali ya ulaya kwa sasa na athari zitazopatikana katika uchumi wa dunia, hata kufikia Benki ya Dunia kushauri nchi za ulaya kuelekeza nguvu zaidi katika mipango na miradi yao ya muda mfupi na muda wa wastani na kuacha kufikiri na kupanga mipango ya kimaendeleo ya muda mrefu.
Nadhani watanzania sasa tunapaswa kuelekeza masikio yetu na macho yetu Dodoma ili kupata uhalisia wa hali yetu kiuchumi na namna tunavyoendelea kuimarika kiuchumi.
Nimefurahishwa na majibu ya waziri wa Nishati na Madini Mhe, Sospeter Muhongo pale aliposema kuwa sasa wanatekeleza mipango ambayo si tu itahakikisha Nishati ya umeme inapatikana Tanzania bali wana-projections kugeuza Tanzania kuwa ni wazalishaji-wauzaji wa Nishati hiyo, na hivyo wamelazimika kuanza kuchimba madini ya Uranium kabla ya Kenya.
Tuendelee kusikiliza Bunge letu litakaloendelea tena saa kumi Jioni.
Post a Comment
CodeNirvana