YAH: TAARIFA KWA MADAKTARI NA KADA ZOTE ZA AFYA NCHINI JUU YA MKUTANO UTAKAOFANYIKA JUMAMOSI, TAREHE 09.06.2012, DAR ES SALAAM
Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kinapenda kuwakaribisha madaktari na kada zote za afya nchini Tanzania siku ya Jumamosi, tarehe 09.06.2012, Dar-es- Salaam katika ukumbi wa KOREA [Korea Cultural Hall] kuanzia saa tatu asubuhi.
Agenda kubwa ya mkutano ni kutoa taarifa ya mrejesho wa mazungumzo kati ya wawakilishi wa madaktari na Serikali.
Itakumbukwa kwamba kikao cha mwisho cha madaktari juu madai yao kilifanyika ukumbi wa Don Bosco na kwenye kikao hicho madaktari waliwatuma wawakilishi wao kwenda kwenye meza ya majadiliano na serikali. Mpaka sasa, jumla ya vikao sita vimeshafanyika na kikao cha mwisho kilifanyika tarehe 31/05/2012.
Hivyo basi MAT inawajibika kutoa mrejesho baada ya majadiliano kufikia tamati na serikali kutoa msimamo wake.
Karibuni nyote!
IMETOLEWA NA CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA
Source: http://www.wavuti.com
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana