Loading...
Nape Nnauye atoa wito wa kuwakaribisha wote Jangwani leo
Chama Cha Mapinduzi, ndio Chama pekee ambacho kimepewa dhamana ya kuongoza Nchi hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ridhaa hii inatoka kwa wananchi walioiamini na kuichagua.
Wananchi hawa wanayo haki ya msingi ya kuhoji na kuiuliza CCM imetekeleza nini katika ILANI yake, kwa kiasi gani inaisimamia serikali yake katika kuhakikisha Maendeleo ambacho ndio lengo kuu la Uongozi wetu yanapatikana kwa wananchi wote kwa ujumla na si mmoja mmoja. Chama kikiwa kimya watatokea watu wasiojua kitu wala wasio na ufahamu wa yale yanayoendelea katika Chama lakini pia Katika serikali katika utekelezaji wa ILANI. Wapo wengine wataopotosha na kusambaza propaganda za kutengeneza chuki na kubeza mafanikio ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi chote ambacho kinaongoza Nchi hii.
Lakini, Chama Cha Mapinduzi akiwezi kuacha haya yaendelee kutokea, ni kwa namna hii tunawaambia wanachama wetu na wananchi kwa Ujumla ni ni hasa Chama Chao kimefanya, kinafanya na nini kitafanya katika mikakati yake na mipango yake kulingana na vipaumbele vilivyoainishwa katika ILANI yake .
Alasiri ya Jumamosi ya Leo,tarehe 09-06-2012. Chama Cha Mapinduzi kitafanya Mkutano wa Hadhara wenye maudhui ya Kutoa Msimamo Wa Chama Juu ya Masuala Yanayogusa Mustakabali wa Taifa.
Natumia fursa hii kuwakaribisha wote Jangwani Alasiri ya Leo.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Post a Comment
CodeNirvana