Loading...
Wabunge wa Bunge La Afrika Mashariki
Spika mpya wa Bunge la Afrika Mashariki Mh.Zziwa kutoka Uganda.
Spika Margaret Zziwa,wa bunge la EALA , akisindikizwa na Spika aliemaliza muda wake Abdirahin Abdi mara ya baada ya kuchagulai hapo jana Arusha.
Mh.Samuel Sitta ambae ni muwakilishi wa Tanzania
Mbunge Shy-Rose Banji akila kiapo chake.
Mh.Charles Makongoro Nyerere
Mh. Alhaji. Adam Kimbisa.
Dkt Twaha Issa Taslima
Mh.Nderkindo Perpetua Kessy
Mh.Abdullah Alli Hassan Mwinyi
Mhe Bernard Musomi Murunyana
Mhe. Anjela Charless Kizigha
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hulo.
Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.
Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose SaddrudinBhanji.
Wengine ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya,Mh.Nderkindo Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.
Wabunge hao wameapisha pamoja na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na katika picha juu ni Waziri wa Afrika Mashariki na mbunge wa Urambo Mh Samwel Sitta akiapa katika bunge hilo jana jijini Arusha SOURCE: FATHER KIDEVU BLOG
Baadhi ya wabunge wa Tanzania wakishiriki katika Uchaguzi wa Spika Bunge la EALA.
Mh.Shy Rose akitoka kupiga kura yake kuchagua Spika wa Bunge la EALA
65% ya budget ya Bunge la EALA inakuwa inafadhiliwa na donors! bado kazi ipo.
Post a Comment
CodeNirvana