Kwa mara nyingine wapenzi wasomaji wangu tunakutana tena siku hii ya
Jumatatu murua katika kilinge chetu hiki cha XXLove kwa kudra za
Mwenyezi Mungu.
Asanteni wadau wote mnaonitumia ujumbe mfupi wa sms na kunipigia simu
kwa maoni na ushauri kuhusu mada ya wiki iliyopita ya Kumbe
Kubembelezwa Siyo Kupendwa.
Kwa maoni yenu ni dhahiri kwamba wengi wenu mmekuwa mkidanganywa hivyo mtakuwa mmejifunza kitu.
Leo nazungumzia mada inayojieleza hapo juu kuhusu ndoa. Nianze kwa
kusema kuwa katika miaka ya hivi karibuni suala la ndoa limekuwa kama
kitendawili f’lani hivi.
Uchunguzi wangu mdogo na wa kawaida umenipa majibu kuwa waolewaji wako tayari kabisa ila waoaji ndiyo wamekuwa ‘michosho’. Hawaeleweki au hawapo tayari.
BADO UNAJIPANGA?
Ninaamini kikwazo kimojawapo kwa vijana walio wengi ukiwauliza watakwambia ‘bado najipanga’.
Ninaamini kikwazo kimojawapo kwa vijana walio wengi ukiwauliza watakwambia ‘bado najipanga’.
Kimsingi hakuna kujipanga kihivyo katika maisha. Unavyoishi ndiyo
maisha halisi, mengine unayoyataka yanaweza yakapatikana au
yasipatikane, inategemea na vile unavyojituma, sambamba na kumshirikisha
mtoaji wa riziki ambaye ni Mwenyezi Mungu. Tukumbuke hakuna namna
tunavyoweza kufanya mambo yetu bila kumshirikisha Mungu.
MAPENZI KABLA YA NDOA
Ishu kubwa zaidi inayochangia kwa vijana wa kiume na kike kutooa au kuolewa, si ishu ya kutokujipanga bali kujiingiza katika tendo lenyewe linalohusisha ndoa kwa maana ya kufanya tendo kabla ya ndoa.
Ishu kubwa zaidi inayochangia kwa vijana wa kiume na kike kutooa au kuolewa, si ishu ya kutokujipanga bali kujiingiza katika tendo lenyewe linalohusisha ndoa kwa maana ya kufanya tendo kabla ya ndoa.
MFANO
Unadhani kwa tabia yako ya umapepe na kutembea na wanaume ovyo, ni nani atakuoa wakati kila mtu anaujua mwili wako? Umri wako ni chini ya miaka 18 ila una msururu wa wanaume, hilo ni tatizo tena kubwa sana.

TABIA YA VIJANA
Kwa tabia yako ya uzinzi, hakuna kijana anayekufahamu atakuwa tayari kukuoa, yawezekana hapo ulipo usiku wa kuamkia leo hujalala kwenu, umekesha kwenye vigodoro, kumbi za starehe au kwingineko. Kama haitoshi, hukohuko ukapitia kwa mwanaume mwingine kulala mbali na yule uliyekuwanaye kwenye muziki.

KAMA NI KUOLEWA
Kama ikitokea ukaolewa, basi ujue mwanaume ameamua tu kujitwisha gunia la misumari au ni mwanaume asiyezijua tabia zako vizuri na mwanaume wa namna hiyo basi atakuwa ametoka mbali na hakuulizia tabia yako kwa wenyeji wake.

KUGAWA PENZI OVYO
Kama utaendelea kugawa penzi ovyo, hakika ni vigumu mno kuwa na ndoa kwa sababu wanaume wanapenda kuonjaonja na kama wakikataliwa kuonja kama walivyodhania uamini mwanamke huyo ndiye anayestahili kuwa mkewe.

Kimsingi hili ndilo tatizo kubwa sana linalokikumba kizazi cha sasa
kiasi cha kusababisha ndoa nyingi kupungua. Kila kukicha vijana
wanabadilisha wachumba kwa kisingizio hakuwa taipu yake, ukimuuliza
taipu gani unayohitaji haijui!
Mpenzi msomaji unadhani ni kwa nini wanaume hawa na wanawake wengi hawaolewi kwa sasa? Tujadili. Tuma maoni yako na yatachapishwa kwenye safu hii wiki ijayo.
Pia usikose kutembelea mtandao wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook na Instagram kwa elimu zaidi kuhusu mapenzi.