CATHERINE MAGIGE(CCM)
Sifael Paul na Brighton Masalu
Upande wa pili! Bunge la 11
liliahirishwa Ijumaa iliyopita ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliwahutubia wabunge huku Waziri Mkuu,
Majaliwa Kassim Majaliwa akihitimisha hotuba kwa kuliahirisha rasmi
bunge hilo hadi Januari 26, mwakani.
Hata hivyo, hiyo siyo hoja wala gumzo
kuu la bunge hilo ambalo linajumuisha wabunge wengi wapya kutoka vyama
mbalimbali, lakini ‘pointi’ kubwa ni jinsi wabunge 15 wanawake ambao
walilitikisa bunge hilo kutokana na urembo wao na kuzua gumzo kubwa.
Wabunge hao warembo a.k.a visu ambao
umri wao bado ni ‘asubuhi’, walikuwa kivutio machoni mwa baadhi ya
wabunge hususan vijana ambao ‘walivunjika’ shingo juu ya wawakilishi
hao.
Ijumaa Wikienda
linakupa orodha ya wabunge hao warembo ambapo waliojulikana kwa
kukimbiza kama akina Halima Mdee wametakiwa kukaa chonjo. Hata hivyo,
wabunge warembo wa kike ni wengi, lakini wafuatao ndiyo ‘shida’ kuanzia
maumbo na sura zao.
CATHERINE MAGIGE (CCM)
Rekodi ya urembo wake haijawahi kuvunjwa
bungeni. Mara zote, tangu alipotinga bungeni mwaka 2010, amekuwa gumzo
kubwa kwa uzuri wake, licha ya kushindanishwa na wabunge kadhaa, lakini
bado ‘anatusua’ vilivyo.
Hii ni mara yake ya kwanza kuingia
bungeni. Uzuri na urembo wake umeonekana gumzo bungeni tangu mwanzo hadi
mwisho wa kikao hicho. Sura, umbo na macho yake vimekuwa kivutio
kikubwa.
ANGELLA KAIRUKI (CCM)
Ukimwangalia vibaya, unaweza kusema ni
shombeshombe. Urembo wa sura yake, umekuwa ukiwapa nyakati ngumu watu
wengi, wakati mwingine kushindwa hata kung’amua kama ana asili ya
Kiarabu au la! Kinachomuongezea sifa katika kilinge cha urembo ni umbo
lake lililojengeka.
ESTER MATIKO (CHADEMA)
Achana na ukali wa hoja zake
anapochangia mijadala. Hiki ni ‘kisu’ kikali kinachovutia bungeni. Umbo
lake la ‘kitoto’, uzuri wa sura na macho ya mviringo, vinamfanya
aonekane mrembo na mwenye uzuri wa kupindukia.
LOLESIA BUKWIMBA (CCM)
Tabasamu lake ndiyo limekuwa gumzo. Sura
yenye uchangamfu imekuwa ikiteka macho ya watu wengi. Kamwe huwezi
kuchoka kumtazama mwakilishi huyo. Mpole kama alivyo, lakini amekuwa
‘akikimbiza’ vilivyo mjengoni.
DK MARRY MWANJELWA (CCM)
Licha ya umri kuanza kumpigia honi
lakini anawafunika wabunge wengi wenye umri mdogo. Urefu na figa nzuri,
vinachangia kwa kiasi kikubwa kumweka kwenye orodha ya wabunge wa kike
wanaotikisa kwa uzuri.
UMMY MWALIMU (CCM)
Hana makuu. Mpole na mwenye aibu wakati
wote, lakini urembo wake unashereheshwa na umbo lake matata. Ana urembo
wa haja unaoyapa macho kazi ya ziada kuitafuta kasoro yake.
CECILIA PARESSO (CHADEMA)
Urembo, uzuri wa umbo lake, urefu, unene wa wastani na sura nzuri vinatosha kumuingiza kwenye orodha hii.
JULIANA SHONZA (CCM)
Umbo lake ni la kawaida, lakini shughuli iko usoni. Achana na sehemu zingine za mwili, ukimtazama usoni tu utagundua ni kisu.
LUCY MAYENGA (CCM)
Ni mrembo wa umbo na sura. Hahitaji
maneno mengi kumwelezea, lakini ukweli unabaki palepale kuwa ni miongoni
mwa wabunge warembo walioupa shida Mji wa Dodoma.
MBONI MHITA (CCM)
Akiwa umbali kidogo kutoka mahali ulipo,
unaweza kumchukulia kawaida! Shughuli ipo akikusogelea. Umbo na uzuri
wake ni habari nyingine.
NEEMA MGAYA (CCM)
Rangi yake ya asili, ngozi laini, umbo
namba nane na ucheshi wake, vinamtetea kuingia kwenye ulingo wa wabunge
hawa warembo zaidi.
VICKY KAMATA (CCM)
Silaha kubwa aliyonayo ni midomo na
macho! Geuza gazeti nyuma, mtazame tena Vicky, unaona? Si umbo, si sura,
si macho, si mdomo, Vicky Kamata ni mrembo. Inatosha kusema hivyo tu.
JESCA KISHOA (CHADEMA)
Ni mrembo anayevutia kwenye viunga vya
bungeni na inawezekana ndiyo maana aliyekuwa Mbunge wa NCCR-Mageuzi,
David Kafulila aliamua kuchukua jumla na kumweka ndani.
ESTER BULAYA (CHADEMA)
Kama unahitaji kumpongeza muumba kwa
kazi njema, wewe mtazame Ester Bulaya, si mrefu, si mfupi, si mweusi
wala si mweupe. Yuko kati kwa kati. Akitembea, kama ni barabarani,
jihadhari na vyombo vingine vya usafiri.
SOURCE:GPL