Askofu Josephat Gwajima
Taarifa hizo zilizozagaa katika mitandao ya kijamii zilieleza kuwa
Askofu Gwajima alifariki dunia katika hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini
Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hizo zilienea kuanzia ya saa tano asubuhi,
zilieleza kuwa Askofu Gwajima alifariki dunia kwa shinikizo la damu.
Hata hiyo, taarifa hizo zilikanushwa vikali na mwanasheria wake, wakili wa kujitegemea Peter Kibatala.
Akizungumza na Nipashe jana, Kibatala alisema taarifa hizo ni za uzushi ambao haelewi chanzo chake.
“Nimesikitishwa na taarifa hizi na nimepigiwa simu nyingi sana leo
kuniuliza juu ya kifo cha Askofu Gwajima na nimebaki nashangaa kwani ni
mzima wa afya,” alisema Kibata.
Majira ya jioni jana picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii
ziliomwonyesha Askofu Gwajima akiwa mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
CHANZO:
NIPASHE