Msanii
Nuh Mziwanda amefunguka baada ya kuachana na mwandani wake Shilole, na
kusema kuwa Shilole hakuwa mtu mzuri kwake, ndiyo maana ameamua kufuta
hata tatoo ya jina lake aliyoichora.
Nuh
ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo
kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba wakati yupo kwenye
mahusiano na Shilole alishindwa kuonesha undani wake, ambao amekuja
kuujua baada ya kuachana na penzi kuisha.
“Baada
ya mapenzi kuisha mi nimekuwa adui yake, amehack acount yangu ya
instagram najaribu kuwacheki wa kurudisha acount yangu wanashindwa
kunirudishia anabana kila sehemu, kuna vitu ananifanyia vidogo vidogo
ambavyo nimefanya kugundua kuwa hakuwa mwanamke mzuri kwangu, alikuwa
anashindwa kuonesha true colour yake nimekuja kuijua baada ya kuachana
naye”, alisema Nuhu.
Pia
Nuh Mziwanda amesema iwapo wangeachana kwa amani na Shilole
asingelazimika kuifuta tatoo hiyo, kwani ni ukweli usiopingika kwamba
amemsaidia katika maisha yake.
“Mi
ningeiacha tatoo kama Shishi ningeachana nae poa, kila mtu na maisha
yake fresh tukionana tunasalimiana hakuna noma, lakini mwenzangu kwenye
interviews anasema, akiitwa kwenye interview anaongea hiki kwamba mimi
sina kitu, sijui nashindwa kusurvive nakula magengeni, anaongea vitu
vingi ambavyo anajaribu kutoa fan base yangu, angekuwa mtu mzuri baada
ya kuachana naye tatoo ningeiacha kwa sababu ningejua bado kabaki kuwa
rafiki yangu na ni mtu ambaye alinisaidia”, alisema Nuh.
Pamoja
na hayo Nuh amesema yeye binafsi hana chuki na msanii huyo ambaye
alikuwa naye kwenye mahusiano, na kwa sasa ana mahusiano mengine ambayo
asingependa kuyaweka wazi.
Mimi
sina ubaya na Shishi , sina ugomvi naye na wala sitaki kufikiria kuja
kuwa na bifu naye, nipo kwenye mahusiano lakini siwezi kuweka wazi
mahusiano kwenye mitandao ya kijamii, sababu ni mke wangu yuko kwenye
moyo wangu, hayupo instagram wala kwenye mitandao ya kijamii”, alisema Nuh.