Liverpool vijogoo vya Anfield wameanza vyema kampeni zao kwenye michuano ya Europa League
hatua ya 16 bora baada ya kuiangushia kipigo Manchester United cha bao
2-0 kwenye uwanja wa Anfeild jana usiku.
Ulikuwa usiku mzuri kwa mashabiki wa Liverpool usiku wa jana na kuwa mchungu kwa Mashabiki wa Manchester United waliosafiri kuja kuiangalia timu yao wakizani wataendeleza ubabe wao kwa Liverpool lakini haikuwa hivyo.
Goli la pili lililoimaliza Manchester United usiku wa jana likifungwa na Firmino.
.....
Kikosi cha Jurgen Klopp kilitawala mchezo huo kwa asilimia kubwa ya
mchezo huo wa kwanza kati ya timu hizo za Premier League giants huku
kocha huyo wa kijerumani akifurahia ushindi wake dhidi ya United.
Daniel Sturridge aliipa Liverpool goli la kuongoza dakika ya 15 kwa
mkwaju wa penati baada ya Memphis Depay kumfanyia madhambi Nathaniel
Clyne kwenye eneo la hatari penati ambayo imezua mjadala mkubwa kwenye
mitandao ya kijamii wadau wakikosoa kwamba ilikuwa ni nje ya penalty
box.
Roberto Firmino akaongeza bao jingine kwa shuti kali la karibu zikiwa zimesalia dakika 17 pekee mchezo huo kumalizika.
United haikutengeneza hata nafasi moja ya kufunga, ubora wa golikipa
wao David de Gea ndiyo umeikoa United kuchezea idadi kubwa ya magoli
kwenye mchezo huo baada ya mlinda mlango huyo wa Hispania kuokoa michomo
mingi.
Rekodi zilizowekwa kwenye mchezo huo:
- Manchester United hawajashinda mchezo wowote wa ugenini kati ya michezo yao sita iliyopita kwenye hatua ya moano ya michuano ya Ulaya, wamepoteza michezo mitano kati ya hiyo.
- United imepata clean sheet moja kwenye mechi 10 walizocheza kwenye uwanja wa Anfield kwenye mechi za mashindano yote.
- Daniel Sturridge amefunga magoli matano na ku-assist goli moja kwenye mechi saba dhidi ya United kwenye mashindano yote.
- United wamepigiwa mashuti nane on target dhidi ya Liverpool, mashuti mengi zaidi kuziuwa na klabu hiyo ndani ya mechi moja msimu huu.
- Roberto Firmino amefunga magoli matatu mfululizo kwa mara ya kwanza kwenye mechi za Liverpool.