Na Dastan Nehemia
Usajili wa Mbwana Samatta kutoka TP Mazembe kwenda KRC Genk ya
Ubeligiji ni hatua nzuri kwa wachezaji chipukizi wa Tanzania na vilabu
vya soka kutumia usajili huu wa Samatta kama daraja na kuvuka na kwenda
mbele kisoka.
Mbwana Samatta baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa
wachezaji wa ligi za Afrika ni hatua kubwa kwani vilabu vikubwa duniani
sasahivi macho yao yako nchini kutazama wachezaji wengine, ndio maana
hata Thomas Ulimwengu amekuwa akiwindwa na vilabu vingi hii ni kutokana
na Samatta kufungua njia.
Vilabu vikubwa duniani huamini mchezaji mmoja bora anapopatikana
kutoka nchi fulani huwa kuna wengine zaidi ya mia moja nyuma yake ni
kama mgodi wa madini hauwezi hutoa almasi moja tu lazma ziwepo nyingine
na ni kama kwenye muziki wa kizazi kipya baad ya diamond Plutnumz kuanza
kupata tuzo za kimataifa njia pia zimefunguka kwa wasanii wengine kama
Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz kupa tuzo za kimataifa pia.
Juhudi zikiongezeka kwa wachezaji baada ya mwaka mmoja tu tusishangae
kuona chipukizi kama Haji Ugando, Hassan Kessy, Ramadhani Singano
(Messi) na Haji Mwinyi wakiwa Italia au Ubeligiji wakicheza mpira katika
klabu mojawapo.
Jambo la msingi ni vilabu vyetu vya hapa nchini kujifunza kutoka kwa
klabu kama TP Mazembe ambayo imefanya uwekezaji wa kweli na inaongozwa
na viongozi makini wa soka na ndiyo maana inafanya vizuri katika
mashindano ya kimataifa na hiyo ndiyo sababu inayopelekea wachezaji wao
kupata kuonekana na vilabu vya Ulaya.
TP Mazembe kwa kumuuza Mbwana Samatta kwenda kwenda KRC Genk
waamepokea Tsh billion 1.6 pesa ambayo ingepata moja vilabu vya Tanzania
ingesaidia katika uwekezaji hasa ujenzi wa viwanja vyao binafsi na
kusaidia kuongezeka upatikanaji wa mapato.
Endapo vilabu vyetu vya Azam FC, Yanga SC na Simba SC, vilabu ambavyo
vinasemekana vinawachezaji bora vikipata nafasi ya kufanya vizuri
kwenye klbu bingwa Afrika na kombe la shirikisho basi wachezaji wa
kitanzania watapata nafasi kuonekana na kununuliwa na klabu kubwa za
Ulaya hili litasaidia kukuza soka letu na kutengeza timu nzuri ya taifa.
Lakini je vilabu vyetu vya Simba na Yanga vinapigania wachezaji kutoka kwenda kucheza Ulaya?
Sababu mara nyingi tumekua tukiona hivi kwa matakwa yao binafsi
vikiwanyima fursa wachezaji wao kujiunga na vilabu vikubwa, lakini
endapo wangetambua umuhimu wa wachezaji hawa kwenda vilabu vikubwa basi
vilabu vyetu vingekua vikipigana kuwapeleka wachezaji wao kufanya
majaribio mara kwa mara kama vilabu vya Afrika Magharibi nchi kama
Nigeria, Ghana na Senegal kucha kutwa wanapeleka wachezaji wao nchi za
Ufaransa, Italia, Ubeligiji na Uholanzi kufanya majaribio katika vilabu
mbalimbali kwa gharama zao.
Hivyo basi watanzania tusisherekee tu Mbwana Samatta kwenda Ulaya bali tumtumie kama daraja la kupitia wachezaji wengine.
0655995405