Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Kujitoa kwa Wekundu Taska

Kujitoa kwa wekundu wa msimbazi katika mashindano ya Taska huko Mwanza kumezusha malumbano miongoni mwa wadau na wapenzi wa soka kuwa ni kwanini wamejitoa.
Vingozi wa wekundu hao wanasema kuwa wakati wa kufanya kazi kisomjo somjo sasa umekwisha.Mambo yawe wazi toka mwanzo na yawe kati ya mdhamini na Klabu sio iwe TFF na Mdhamini baadae yafike kwa klabu hapa klabu inakuwa haielewi ni nini kimezungumzwa kati ya pande mbili hizo.
Kwani hata maslahi yao hayatazingatiwa.
Kujitoa huku kwa Simba ni somo kwa vilabu vyote hapa nchini.
Kwani baadae Wadhamini watakuwa makini katika udhamini kwa kuzitendea haki klabu.Haki hiyo ni kuwapa fedha ya uhakika iili waweze kujiandaa vizuri namapema.
Simba wanasema hawawezi kujindaa kwa siku moja kabla ya mashindano ,kwani Wadhamini waliahidi kuzilipa timu zote fedha kuanzia siku moja kabla ya kipute siku nyingine walizokaa kambini watajiju wenyewe.
LAkin yapo maswali .Je ni kweli Shirikisho linapata mgawo mkubwa kuliko vilabu?
Vilabu vinafaidika vipi na mashindano haya kwa kuangalia faida kwa mchezaji na kwa timu kwa ujumla?
Au ndio mambo ua kibongo bongo au kisomjo somjo?
KAribu kijiweni
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top