Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Open University Baash Part.

Kesho tarehe 3.8.2007 kutakuwa na patizii la kukata na mundu pale kigamboni kuanzia mida ya saa tatu za asubuhi mpaka majogoo.Pati hili litaanza kwa michezo mbalimbali kama rede,netiboli,nk.Pia kutakuwa na muziki ukiambatana na nyama choma hiyo ni mida ile ya jioni hapa unajichomea mwenyewe nyama yako bila ya ajizi.
Dhumuni haswa ni katika kuwakutanisha vijana ili waweze kubadilishana mawazo baada ya kazi ngumu ya kulijenga taifa kwani vichwa navyo vikichoka vinauma kweli.
Lakini wakati wazo hili la kwenda kukutana likiwa vichani mwetu tumesikia kuwa kuna mtanzania mwenzetu ambaye mke wake amejaliwa kupata watoto mapacha pale Temeke hospitali habari yenyewe bofya hapa uisome zaidi http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=802
Familia hii INAWEZA kulia wakisikia kuwa wengine wako tayari kujichangisha ili waende KUJIPUMZISHA huku wao wakishindwa hata kupata kifungua kinywa cha uhakika.
Nwapongeza sana Mwananchi kwa kusimamia suala hili na hatimaye yule mzazi kuweza kutabasamu kwa kuwezeshwa kupitia kwenu.
Jamii nzima tunayo maswali ya kujiuliza huko tunakoenda kukoje.
Je ungekuwa wewe ni kiongozi wa pati hii ungefanyeje ?
Ungeendelea na mipango ya sherehe yenu ?
Pia ungeliangaliaje hili suala la Temeke?
Iwapo ungeendelea na mipango yenu kama kawaida,NI lipi ungelipendekeza kwa jumuiya yako hiyo?
Karibuni sana Kijiweni
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top