Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Nakumbuka wakati ule shuleni.......

wakati tuko shule ya msingi kuna mambo ambayo nikikumbuka hushindwa kupata jibu haswa nini kilifanya hayo kuwa yanatokea.Unaweza nawe kuwa yalitokea kipindi hicho ?
Unakumbuka walipo kuwa wanakuja WAKAGUZI toka wilayani ?
Au mlipokuwa mnaambiwa kesho kuna maandamano ?
Mi nakumbuka kama kuna wakaguzi wanakuja basi wote darasani tutanyoosha mikono pale tutakapoulizwa swali.Kwa kuwa mwalimu anatufahamu vizuri basi anajua ni nani wa kujibu hilo swali.
Kwani wengine watamwangusha.
Lakini anayetakiwa kuwaelimisha hawa waelewe si yeye Mwl.
Je haya yanaendelea mpaka leo?
Je huu ndio ukaguzi au ni funika kombe mwanaharamu apite?
PIA wakati tunaenda kwenye maandamano pamoja na njaa tulikuwa tunafua nguo na kupiga pasi.
Siku hiyo ni wote mpo safi yule ambaye ni mchafu au hakufua kwanza pale pale shule unapita ukaguzi wa HATARI walimu wote wanatoka kukagua wakiongozwa na yule Mwalimu mkali kuliko waote ndio maandamano yanaanza.
Wee acha
We unakumbuka ?
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

3 maoni

Mzee wa Kijiweni,hapa umenikumbusha ,mbalisana.
Nakumbuka kipindi nasoma MAGADU PRIMARY SCHOOL Morogoro katika ile milima ya waluguru,udongo mwekundu,shati jeule,kaptula ya blue halafu haina mifuko wala zip,Duh tumetoka mbali.Kiatu usisema,sehemu ya kiatu upande wa kisigino ngoja tu nikae kimya.

Fikiria baridi ya morogoro,umevaa sharti bila fulana ndani,ukifika tu shuleni mchaka mchaka.

Kati hali kama hii utajibu swali kweli au utaishia kunyanyua mkono wa kushoto juu

Reply

Swadakta Ras hapo na kbaridi nazani hata kamasi kwa mbali lilikuwa lintoka huku ukiliburuza au kulipangusa kwa mkono baadae linaganda mkononi wacha we.....

Reply

Nahisi jambo hili linaendelea. Umenikumbusha mbali sana.

Reply
CodeNirvana
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top