Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

Kwanini tunaomba?

Kila ukiangalia televishani utakuta watu au mtu anasema tunaomba viongozi au serikali itujengee daraja,shule,zahanati nk.
Ukisikiliza Radio utasikia,Wakazi wa ......wameiomba serikali iharakishe kuwaletea maendeleo...nk.
Hata mikutano mbalimbali watru ni kuomba kutatuliwa matatizo yao.
Hata makazini Lugha ni hii tu.
Hata viongozi wetu nao tunatakiwa kuwaomba kujenga shule kijijini kwako ?
Pia Diwani,Mbunge nk nao tuwaombe nao kutuharakishia maendeleo?
Nami NAOMBA USIACHE KUTOA MAONI YAKO KWENYE BLOGU YANGU
Karibu kijiweni
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

8 maoni

Mzee wa kijiweni nakubaliaana na wewe licha ya kuomba maoni ni haki yako na haki ya wasomaji kuacha maoni katika blogu yako.
usikate tamaa kwani safari ndio kwanza imeaanza,kaza buti mkuu.

Reply

Hivi ni kweli mtu ukizoea kuomba unakuwa mjinga? na yule mtu anaendekeza kukupa kila siku nae anakutengezenea mazingira ya kuja kuwa mtumwa wake baadae.
Mfano mzuri ni hii misaada tunayoomba kila siku na hawa jamaa wanatupa misaada lakini hawatufundishi ya sisi kujitegemea.Kwenye sekta muhimu kama ya elimu wameweka ngumu.
Hawatufundishi jinsi ya kuvua samaki wanatupa samaki.
Hivi ni jukumu lao kutufundisha?

Reply

Mzee Ndabagoye umesema,
tunapenda sana kuomba
yani neno OMBA,OMBA,OMBA,OMBA
Nani alaumiwe?
je ni sisi raia wema
je ni viongozi wetu
je OAU,AU,EAC
je ni UN
je ni USA
je ni EU?

Wanablogu tuchangie.HII OMBA OMBA IWE MWISHO mara utasikia naomba mzee Simon unitumie..........

Reply

Si jukumu lao kutufundisha namna ya kuvua samaki HILI ni jukumu letu.Wakitufundisha si tutawakimbia ? Wao wanafurahia sie kuendelea kuomba.
NA tumeambukizwa na sie wanakijiji kiasi kwamba yale majukumu ya viongozi au niseme wajibu wa viongozi kwetu sisi tunafanya kuomba>Wajibu wa mbunge au Kiongozi kwako wewe nini?
AU dhamana aliyokabidhiwa kwa kuongoza ni ipi?
KWANINI anaposhindwa kuutekeleza wajibu wake kwako TUNAMUOMBA AUTEKELEZE ?
Wkati ulimtuma wewe.
Ndabagoye amezungumzia kufundishwa kuvua samaki sio kuletewa tu samaki.HIi ni muhimu kwa kila jamii kwetu hapa nchini kuanza na familia yako au jamii iliyokuzunguka.Hii itasaidia kuacha tabia ya kusubiri kuletewa na kuanza kufuata sasa huko vilipo.
Karibu kijiweni

Reply

Kuomba kama kuomba hakuna tatizo lakini unaweza kuangalia katika mitizamo tofauti tofauti.Huwezi kuwa unaomba kila siku wakati una kila njia ya kukufanya usiombe.Raisi wetu anaomba misaada kama njia ya kuwakwamua watu wake lakini kasahau kuwa muda wa kuzungusha bakuli nje angetumia gharama hizo kwa kuzalisha hiki kidogo kilichopo.
Ziwa tunalo,ndoano zipo,wavuvi wapo kwanini tunaomba samaki hata kwa wasio na ziwa?
Rasta&Chediel tukianza kutafuta mchawi hatutafika popote cha muhimu tuanze sisi wenyewe kupiga vita ujinga,umaskini na N.k ili kupunguza utembezwaji wa bakuli kwa "wazungu"

Reply

NI kweli yabidi kupiga vita hao maadui ili tuweze kusonga mbele.Tupunguze umaskini kwa vitendo si kupiga domo kila kukicha huku watu tunataabika

Reply

Naomba kutoa maoni yangu.

Tusipokuwa tunaomba tunapenda kusema HAPANA "tukipewa" fursa kutoa maoni: Vyama vingi HAPANA, Shirikisho la Afrika Mashariki HAPANA, Uraia wa nchi mbili HAPANA. Kila kitu HAPANA bado muda haujafika. Muda utafika lini?

Naomba kuwakilisha.

Reply

Muda ndio huu wa kupambana.Wenzetu wanaweza kuwa walianza mapema na kwa kuwa dunia ya sasa inatufanya lazima kufungua mipaka ili uweze kushirikiana na wenzako kwa ajili ya kukuza uchumi wetu na kujiletea maendeleo TUTAJIJFUNGIA NDANI MPAKA LINI ?.
Muda tutakao kumbuka kufungua milango kwqa maana ya kujiunga na shirikisho tutakuta wenzetu tayari walishapiga hatua kutoka pale tulipokataa kukaa nao kwenda hatua kubwa zaidi na hapo hatutakuwa na muda watatuvamia kama nzige.
LAKINI ni jukumu la kila mmoja wetu kwa mtu mmoja mmoja kujitayarisha kwa shirikisho.
Karibu kijiweni

Reply
CodeNirvana
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top