Loading...
Barcelona na Chelsea NANI Mbabe leo ?
Chelsea wakijifua tayari kwa mtanange hapo leo usiku katika mchezo nusu fainali ya pili katika Uwanja wa Nou Camp mjini Barcelona watakapoonyeshana kazi na Barcelona FC huku wakiwa na faida ya goli moja.
Wachezaji wa timu ya Barcelona wakijifua kwa ajili ya mpambano wao na Chelsea FC leo usiku katika mpambano unaotajiwa kuwa mkali katika uwannja wa NOu Camp ambapo watajaribu kupooza machungu ya kufungwa na Real Madrid mwishoni mwa wiki huku wakitakiwa kutetea Taji la Mabingwa wa Ulaya ambalo wao ni Bingwa pia wakiwa wako nyuma ya goli moja walilofungwa huko London na Chelsea.
Leo nani atatoka akicheka Chelsea ambao wana goli moja kibindoni na wakiwa na nafasi finyu ya kushiriki Ligi ya Mabingwa mwakani kwani mpaka sasa wako nafasi ya tano na wakiwa wameingia Fainali aya FA au Barcelona ambao wanakaribia kuutema Ubingwa wa ligi ya spain kwa Real Madrid ? Mimi nawe tusubiri tuonee..
Post a Comment
CodeNirvana