Loading...
Home » Unlabelled » Freeman Aikael Mbowe awaandikia Vijana Waraka kwenye ukurasa wake wa Facebook asema...
Freeman Aikael Mbowe awaandikia Vijana Waraka kwenye ukurasa wake wa Facebook asema...
Ni wakati wako kijana, Historia
inaonyesha wazi kuwa
hakuna mwanasiasa mashuhuri
hapa duniani aliyeanzia siasa
akiwa mzee, chimbuko la
mwanasiasa bora lazima lianzie
kwenye harakati za ujana hasa
ikizingatiwa kuwa moja ya sifa
za mwanasiasa bora lazima awe
jasiri.
Awe mtu aliyejitoa kwa dhati
kupinga vitendo vyote
dhalimu,awe mzalendo
anayeipenda na kuitetea nchi
yake wakati wowote, awe
kiongozi anayechukia ufisadi,
rushwa, uongo, uchochezi na
aina yoyote iwayo asiwe
mbaguzi na mwenye kuunda
makundi ya chuki na fitina.Hapo
ndipo chimbuko la mwanasiasa
bora linapoanzia na kikubwa
zaidi lazima mtu wa aina hiyo
awe na uchungu mkubwa dhidi
ya binadamu wenzake
wanaopenda kukiuka haki za
binadamu wenzao kwa ajili ya
manufaa yao binafsi na wale
wanaopenda kujilimbikizia mali
huku wengine wakifa kwa shida.
Mwanzo na dalili za kumuona
mwanasiasa bora ndipo
zinapoweza kuchambuliwa na
sifa hizo na nyingine nyingi
ndizo zilizowazalisha wanasiasa
na wanaharakati wengi wa haki
za binadamu ambao kwa
ushawishi wao wamefanikisha
mapinduzi ya kiuchumi ndani ya
nchi zao.
Wale walioamua kujiingiza
kwenye siasa kwa lengo la
kutafuta utajiri ndio hao hao
waliochangia kuifikisha nchi hii
hapa ilipo na hawana sababu
zozote za kusifia mafanikio
wanayoyataja leo kuwa
yametokana na uongozi wao
uliotukuka kumbe kazi
waliyoifanya ndio hii inayoibua
kwa kasi wanasiasa vijana.
Ukweli utabaki pale pale kuwa,
Rais wa awamu ya kwanza wa
nchi hii, Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere alianza siasa
akiwa kijana mbichi, alibebwa na
sifa zote nilizozitaja hapo juu,
alikuwa jasiri, aliipenda nchi yake
na watu wake na hakuwa hata
na chembe ya ubaguzi.
Kwa kuwa dhamira ya kweli
ilimuongoza katika
ukweli,uadilifu na kujitoa zaidi
kwa ajili ya kupigania haki za
wanyonge hakuona shida
kupoteza kazi yake ya ualimu ili
aingie kwenye siasa, alibaki
kuwa mwalimu bora na
atakumbukwa daima kama
mwalimu.
Post a Comment
CodeNirvana