Naomba nafasi nami hapa Kijiweni Leo
Kwanza nianze kumpongeza sana Mh.John Mnyika kwa Ushindi wake mie nauita wa Pili na ni mmoja wa watu waliofurahia ushindi huo jana.Hongera sana Kaka yetu unastahili ushindi huo ni Nani asiye jua umahiri wako pale Bungeni.
Lakini leo naomba nafasi kuuliza swali langu baada ya kuchunguza Picha nyingi sana kuanzia jana kwenye Blogu hii ya Kijiweni Pia magazeti mengi leo nayo yana Picha hiyo.Mh.John Mnyika anaeonekana kabebwa juu kwa furaha hapo juu na mwenye tabasamu na bashasha tele Mguu mmoja hauna Kiatu..!!
Ndio maana nauliza kiatu cha Mh.Mbunge alichukua nani au kilianguka katika harakati hizo za furaha aliyostahili ? Maana mguu mmoja hauna Kiatu.
Tufurahie wote ushindi huo na Tumpongeze sana Mh.John Mnyika.
NI mimi nisiye kosa Kijiweni.
Juma Kombo
Arusha
Loading...
Post a Comment
CodeNirvana