Loading...
Taswira shamrashamra Ushindi wa John Mnyika
Kwa mbali watu wakiserebuka baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali mashtaka matano yaliyokuwa yana mkabili Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika hivyo wana CHADEMA walikuwa wengi Mahakamani hapo kulipuka kwa furaha na kuingia Barabarani kushangilia ushindi wa kesi hiyo.
Shamrashamra zikiendelea hapo..
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiteta na waandishi wa habari nje ya Mahakama kwa kuwashukuru wananchi wote waliokuwa bega kwa bega na Mh.Mnyika katika kipindi chote cha kesi hiyo.
Madai hayo yalikuwa kama ifuatavyo:
-Kuwepo tuhuma za kashfa kuwa mlalamikaji aliuza jengo la Umoja wa Wanawake, UWT.
-KUbadilishwa kimakosa kwa kura katika formu za matokeo ya Ubunge
-Kuwepo kwa watu katika chumba cha majumuisho ya kura
-Matumizi ya tarakilishi(Laptop) ya mlalamikiwa wakati wa kujumlisha kura
-Ukiukwaji wa taratibu za kisheria katika uchaguzi ambazo zilisababisha kuwepo kura hewa 14,854
Post a Comment
CodeNirvana