Zaidi
ya vijana mia tatu wajitokeza katika usaili wa Onesho la Swahili
fashion week ulifanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Colosseum
iliyopo Oster bay jijini Dar es Salaam.Mwitikio ulikuwa mkubwa sana kwa
vijana ikiwa ni kutaka kushiriki katika onyesho hilo linalozidi kukua
zaidi kwa kuhudhuriwa na wanamitindo wa kimataifa hapa nchini.
Akiongea
katika usaili huo Mwanamitindo maarufu nchini Mustafa Hassanali ambaye
ni mwasisi wa shindano hili amesema kuwa umaarufu wake umekuwa
ukiongezeka mwaka hadi mwaka kwa kuongezeka wanamitindo wa
kimataifa,washiriki,wafuatiliaji wake na wadhamini
“Swahili
Fashion Week ni jukwaa kubwa la mitindo ya mavazi la kila mwaka katika
ukanda wa Afrika mashariki na kati kwa sasa. Huu ni mwaka wa nane sasa,
ambapo Swahili Fashion Week imekuwa ni Jukwaa la wanamitindo na
watengeneza vipodozi vya urembo kutoka katika nchi zinazoongea Kiswahili
na bara zima la Afrika kwa ujumla kuweza kuonesha vipaji, kutangaza
ubunifu wao na kukuza mtandao wa mawasiliano ya kibiashara ndani na nje
ya nchi kwa wadau wa mitindo.
Hili limelenga kuhamasisha ukanda huu wa
Afrika Mashariki na Kati kwamba ubunifu wa mavazi ni njia moja wapo ya
kujipatia kipato na wakati huo huo kukuza bidhaa zinazotengenezwa
Afrika(Made in Africa concept na shindano hilo ltaanza mnamo disemba
4-6)”.Alisema Hassanal
Naye
Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wa
Onyesho hilo kwa miaka nane imesema adhima ya kampuni kuendelea
kusaidia kuboresha michezo na Sanaa nchini kwa kuwa inaamini kupitia
fani hizi watanzania wengi wanaweza kunufaika kwa kupata ajira na
kuwezesha serikali kupata mapato kwa njia ya kodi.
“Sisi
kama Vodacom Tanzania tunaamini fani hii ya ubunifu wa mitindo na
mavazi kwa kiasi kikubwa inaweza kuongeza ajira nchini na kuinua vipato
vya wajasiriamali wengi kama ilivyo michezo mingine ndio maana kila
mwaka tunajitosa katika udhamini wa mashindano haya yenye mwelekeo wa
kubadilisha maisha ya wasajiriamali wa Tanzania kwa maisha yao kuwa
murua”.Alisema
Mmoja wa majaji katika Usaili wa
Swahili Fashion week uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
akimuuliza swali mmoja wa wanamitindo waliofika katika usaili huo.Ambapo
wanamitindo waliochaguliwa katika Usaili huo watapata frusa ya
kushiriki katika kuonesha mitindo mbalimbali katika Onesho hilo
linadhaminiwa na Vodacom Tanzania litakalo fanyika kuanzia Disemba 4-6.
Mariam Rajabu na Regina John wakipita
mbele ya wanamitindo wenzao wakati wa Usaili wa Swahili Fashion week
uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,Ambapo wanamitindo
waliochaguliwa katika Usaili huo watapata frusa ya kushiriki katika
onesha mitindo mbalimbali katika onesho hilo linadhaminiwa na Vodacom
Tanzania litakalo fanyika kuanzia Disemba 4-6.
Mwanamitindo
maarufu nchini na Mwasisi wa shindano la Swahili Fashion week,Mustafa
Hassanali(wapili toka kushoto waliokaa)akisalimiana na Meneja Uhusiano
wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wakati wa Usaili
wa Swahili Fashion week uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam,Ambapo wanamitindo waliochaguliwa katika Usaili huo watapata
frusa ya kushiriki katika onesha mitindo mbalimbali katika onesho hilo
linadhaminiwa na Vodacom Tanzania litakalo fanyika kuanzia Disemba 4-6