Featured

    Featured Posts

    Social Icons

    .
Loading...

TOTTENHAM YAIKALIA KOONI LEICESTER CITY YAIPIGA STOKE CITY BAO 4-0






Mbio za ubingwa wa Ligi maarufu zaidi duniani ya EPL zinaingia katika hatua tamu sana baada ya hapo jana Tottenham kupunguza pengo la pointi na vinara wa ligi hiyo  Leicester City na kufikia pointi tano baada ya kuifunga Stoke City bao nne kwa bila.

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane na Dele Alli ndio walikuwa mashujaa jana  baada ya kuifungia mabao mawili timu yao katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Stoke City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Britannia.Sasa timu hiyo inafikisha pointi 68 baada ya kucheza mechi 34 na kuendelea kukaa nafasi ya pili nyuma ya Leicester City yenye pointi 73 za mechi 3.

CHANZO:Daily Mail
 

Ukweli wa kaka’ke Diamond kubaka Sweden

rommy
Kaka wa staa wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Rommy Jones.

STORI: Musa Mateja, Wikienda
Dar es Salaam: Mwisho wa utata? Hatimaye ukweli juu ya sakata la kaka wa staa wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Rommy Jones umeanikwa ndani ya Ijumaa Wikienda ambalo ni namba moja kwa habari za mastaa ndani na nje ya Bongo.


Kabla ya gazeti hili kuchimba undani wa msala huo, kulienea tetesi mbalimbali kuwa Rommy ambaye ni DJ rasmi wa Diamond na mmoja wa wafanyakazi wa Wasafi Classic Baby (WCB) kuwa amebaka kisha kukimbia nchini humo bila kuelezwa undani wa tukio hilo.

WIKIENDA MZIGONI
Katika kusaka undani wa sakata hilo, wikiendi iliyopita Ijumaa Wikienda lililazimika kuzungumza kwa nusu saa na Meneja Matukio ya Kimataifa wa Diamond, Sallam Sharaff.

Akisimulia kilichotokea, Sallam alisema kuwa maneno yaliyozagaa mtaani na kwenye mitandao ya kijamii yalielemea kwenye ushabiki na hata yanavyoelezewa hakuna anayetambua undani wa tukio hilo lilivyojiri.

Sallam alisema, ukweli wa kila jambo wanafahamu zaidi familia ya Wasafi, hasa wote waliokuwepo kwenye Ziara ya Ulaya.

BOFYA HAPA KUMSIKIA SALLAM
“Mara kadhaa nimekuwa mzito sana kuongelea suala la Rommy Jones kufuatia baadhi ya watu kulichukulia tofauti kabisa na ilivyotokea.

“Ishu hiyo ni kweli ilitokea lakini ninachoweza kusema ni kwamba ulikuwa ni mchezo mchafu ambao ulilenga kuichafulia jina WCB.

“Madai ya Rommy Jones kubaka siyo ya kweli kwa sababu mimi ninachokijua ni kwamba, huyo mrembo aitwaye Debora alikuwa akiwasiliana na Rommy Jones siku kibao yaani ni zaidi ya miaka miwili huko nyuma.

diamond33Rommy akiwa na Diamond.

WATUA SWEDEN, DEBORA AJUA
“Siku tulipofika Sweden tu, Debora alijua kuwa Rommy Jones yupo ‘so’ alimnunulia zawadi ya simu na kumletea kwenye apartments (nyumba za kuishi) tulizokuwa tumefikia na jioni yake akamtumia gari, likaja kumchukua na kumpeleka kwake.

“Kusema kweli sisi huko nyumbani kwa Debora hatukupafahamu ila siku hiyo alimrejesha mapema, tena wakiwa na furaha ya hali ya juu.

“Sisi wote tukaanza kumtambua kama shemeji yetu hivyo jambo la kubakwa hapo sijui linatokea wapi…

“Ukiachilia mbali hiyo, siku iliyofuata mimi nilikuwa nimetoka, baada ya kurudi muda wa jioni sikumkuta Rommy Jones, nilipoulizia nikaambia Debora amemchukua na kuondoka naye.

“Alilala huko na kurudi asubuhi yake maana tulikuwa tunaenda kufanya shoo kwenye mji mwingine.

MCHEZO MCHAFU?
“Ujue ishu hii mimi baadaye nilikuja kugundua kwamba kuna namna ambayo Debora alikuwa akitengeneza mazingira ya kutafuta pesa kwani sheria ya Sweden siku zote ukilala na mwanamke bila ridhaa yake akishitaki unatuhumiwa kuwa umebaka na yeye analipwa kama dola elfu kumi na mbili (zaidi ya Sh. milioni 24 za Kitanzania).

HATA MKEO?
“Hata kama ni mkeo, ukifanya naye tendo la ndoa bila yeye kuridhia na akashitaki, basi wewe utakuwa umebaka na sheria inakufunga huku yeye akilipwa kiasi hicho cha fedha.

salam menejaMeneja wa Diamond, Sallam Sharaff.

KILICHOTOKEA SASA
“Kilichotokea kwa Rommy Jones ni dhahiri kabisa kuwa Debora alitaka kujipatia pesa kwa njia hiyo kwani baada ya kuanza kung’aka kuwa amebakwa, mimi nilimtafuta na kumuomba msamaha maana Rommy Jones hakujua kama sheria ya huko iko hivyo na isitoshe wote walikuwa wamelewa.

“Pamoja na msamaha, Debora aliendelea kuomba afidiwe dola elfu kumi na mbili, mimi nikamwambia nimpatie dola elfu sita lakini aligoma na kutaka hiyo hivyo tukashindwa kuafikiana.

VITISHO KWA DIAMOND
“Baada ya kuona tumeshindwa akaanza kututishia kuwa Diamond ni kaka yake hivyo anahusika na msala huo.

“Kweli polisi walifika na kumkamata Diamond, tukawaambia kuwa Rommy Jones si DJ wetu na kwamba tulimkodi tu na tayari ameshaondoka zake kwao.

“Baada ya kuona hivyo hawakuwa na jinsi, wakamwachia Diamond na sisi tukaendelea na shoo zetu.

“Hayo yote yalitokea tukiwa tumebakiza shoo mbili tumalize ziara hiyo hivyo Rommy Jones akawa ‘wanted’ ndiyo maana aliondoka mapema kurejea Tanzania,” alimaliza kusimulia Sallam.

DIAMOND ANASEMAJE?
Alipotafutwa Rommy Jones simu yake haikuwa hewani lakini kwa upande wake Diamond alisema kuwa Sallam ndiye mwenye mkanda mzima hivyo kama alishafafanua ndivyo ilivyokuwa.

DROO YA NUSU FAINALI KLABU BINGWA ULAYA (UEFA) MAN CITY KUIKARIBISHA REAL MADRID

Man City v Real Madrid 
Atletico Madrid v Bayern Munich

 26-27 Aprili na marudiano 3-4 Mei

DROO YA NUSU FAINALI KLABU BINGWA ULAYA (UEFA) MAN CITY KUIKARIBISHA REAL MADRID

Man City v Real Madrid 
Atletico Madrid v Bayern Munich

 26-27 Aprili na marudiano 3-4 Mei

MKUU WA WILAYA IRINGA AJA KIVINGINE




Mkuu wa wilaya Iringa , baada ya kazi jana alijiunga na wana chuo cha RUCU kucheza mpira wa kikapu

TOUR YA DIOMOND UROPA YAZUA MENGI Dj Rommy Jones Kwenye Kashfa ya Ubakaji Sweden...


Inasmekana alimbaka mdada wakibongo aishie sweden anaitwa Deborah
Shutuma hizo zimewekwa Instagram katika page mbali mbali zinasema Rommy alikuwa na dada huyu nyumbani kwake na kumuwekea kilevi kwenye kinywaji chake akasinzia na jamaa kufanya yake...

Wadaku wanadai Rommy Jones hakumaliza ziara ya chibu chibude huko ulaya kwani alikimbia soo na chat sms zimewekwa hadharani akiomba msamaha
wambeya wanadai meneja wa diamond aitwaye salaam alikuwa radhi kutoa euro 10,000 ili kuua soo ila bidada akakataa....

Kwa Habari zaidi Ingia Page ya Dougie masta huko insta...
or Jamii Forums

HUYU NDIYE SUPER STAR DIAMOND PLATINUMS APATA SHAVU JINGINE LA NGUVU BAADA YA KUTOKA TOUR

Wanasema hela zinaenda kwa wale ambao tayari wanazo. Kwa Diamond kuamka na dili mpya kila kukicha kimekuwa ni kitu cha kawaida.
Na sasa staa huyo amesaini mkataba wa ubalozi wa tomato sauce tunayokutana nayo mara kibao kwenye vile vijiwe vya kulia viepe, Red Gold.
Amesaini mkataba huo jana kwenye ofisi zake za WCB. Huo ni mkataba wa tatu baada ya DSTV, Vodacom.

Alberto Moreno NA 'TATTOO' MPYA


His team may have won the game, but Zidane lost his trousers

FAIZA ALLY..Nampenda Sana Sugu Hata Akitaka Mtoto wa Pili na Watatu Nitampatia....

Baada ya Picha Kusambaa Mitandaoni Sugu Akiwa na Mpenzi wake mwingine, Mama wa Mtoto wake Faiza Ally ambae kwa sasa hawapo pamoja amefunguka mengi nimekuwekea hapa baadhi:


faizaally_ KUMPENDA MTU SIO ZAMBI  TUKANENI TU ! NAUMIA WALA SIKATAI LKN SIO KESI ! NINI HAWARA HATA AKIOA - ACHA MMBONGO HATA AKIOA MALKIA WA UK - BADO SIWEZI KUHUKUMIWA NDIO HIVYO TENA NAMPENDA - PEANENI HABARI - TUKANENI LKN NAMPENDA HIVYO HIVYO NDIO BABA WA MWANANGU HLF SIKUMUIBA....... NAJUA MNATAMANI HATA MWANANGU ASINGE KUWA HUYO NDIO BABA YAKE LKN NDIO BASI TENA MIPANGO YA MUNGU NA BY THE WAY AKITAKA MTOTO WA PILI NTAMPA NA WA TATU PIA.......

Faizaally_ PIGENI TU PICHA KWENYE NYUMBA YA MWANANGU LKN MWENYEWE AKIKUA ATAKUJA - KAMA HAJAWA AMBIA KILA KITU KIKO CHINI YA JINA LA DESDERIA-SASHA - HATA HOTEL MPYA INAITWA DESDERIA  #SHIKAMOO SASHA MBILINYI



Faizaally_ SIFAI NAFAA NDIO MAMA SASHA # THROW BACK MBEYA KWA BABA 🏻️ SEBLENI KWETU NA PAZIA CHAGUO LA MAMA  # KALIENI TU MAKOCHI YANGU #PIGENI PICHA KWENYE MAUA ALIO PANDA MAMA YANGU # NIKIKUA NARUDIIII KWETU #NA HIVI BABA YANGU ANA NIPENDA MTAJAMBIA HEWANI # IN SASHAS VOICE

ALI KIBA AFUNGUKA HAYA KUHUSU DADA YAKE DIAMOND


Msanii wa muziki Alikiba amefunguka kwa kusema kuwa kuna wakati huwa anamkumbuka sana msanii wa kike ambaye ni dada wa msanii Diamond Platnumz, Queen Darleen.

Ali Kiba na Darleen walikuwa washkaji zamani, ambapo Queen Darleen aliwahi mshirikisha Ali Kiba katika wimbo wake, ‘Wajua’ ambao ulifanya vizuri sana.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatatu hii, Ali Kiba alifunguka kwa kusema yeye mwenyewe anamkumbuka Queen Darleen sababu kuna vitu walikuwa wanaendana.

“Queen Darleen alikuwa mkongwe katika gemu na tulikuwa na ukaribu sana,” alisema Ali Kiba. “Kiukweli muda mwingi huwa nina ‘M-miss’ sababu mimi na yeye kuna vitu vingi tulikuwa tukiendana kama washikaji. Muda mwingine akili yangu na yake ni kama sawa vile”,

Kwa sasa wawili hao hawaelewani huku watu wakidai hali hiyo imesababishwa na ugomvi uliopo kati ya Diamond na Ali Kiba.

SAMATTA ATUMIKE KAMA DARAJA KWA WACHEZJI NA VILABU NCHINI

Samatta 77
Na Dastan Nehemia

Usajili wa Mbwana Samatta kutoka TP Mazembe kwenda KRC Genk ya Ubeligiji ni hatua nzuri kwa wachezaji chipukizi wa Tanzania na vilabu vya soka kutumia usajili huu wa Samatta kama daraja na kuvuka na kwenda mbele kisoka.


Mbwana Samatta baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za Afrika ni hatua kubwa kwani vilabu vikubwa duniani sasahivi macho yao yako nchini kutazama wachezaji wengine, ndio maana hata Thomas Ulimwengu amekuwa akiwindwa na vilabu vingi hii ni kutokana na Samatta kufungua njia.


Vilabu vikubwa duniani huamini mchezaji mmoja bora anapopatikana kutoka nchi fulani huwa kuna wengine zaidi ya mia moja nyuma yake ni kama mgodi wa madini hauwezi hutoa almasi moja tu lazma ziwepo nyingine na ni kama kwenye muziki wa kizazi kipya baad ya diamond Plutnumz kuanza kupata tuzo za kimataifa njia pia zimefunguka kwa wasanii wengine kama Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz kupa tuzo za kimataifa pia.


Juhudi zikiongezeka kwa wachezaji baada ya mwaka mmoja tu tusishangae kuona chipukizi kama Haji Ugando, Hassan Kessy, Ramadhani Singano (Messi) na Haji Mwinyi wakiwa Italia au Ubeligiji wakicheza mpira katika klabu mojawapo.


Jambo la msingi ni vilabu vyetu vya hapa nchini kujifunza kutoka kwa klabu kama TP Mazembe ambayo imefanya uwekezaji wa kweli na inaongozwa na viongozi makini wa soka na ndiyo maana inafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa na hiyo ndiyo sababu inayopelekea wachezaji wao kupata kuonekana na vilabu vya Ulaya.


TP Mazembe kwa kumuuza Mbwana Samatta kwenda kwenda KRC Genk waamepokea Tsh billion 1.6 pesa ambayo ingepata moja vilabu vya Tanzania ingesaidia katika uwekezaji hasa ujenzi wa viwanja vyao binafsi na kusaidia kuongezeka upatikanaji wa mapato.


Endapo vilabu vyetu vya Azam FC, Yanga SC na Simba SC, vilabu ambavyo vinasemekana vinawachezaji bora vikipata nafasi ya kufanya vizuri kwenye klbu bingwa Afrika na kombe la shirikisho basi wachezaji wa kitanzania watapata nafasi kuonekana na kununuliwa na klabu kubwa za Ulaya hili litasaidia kukuza soka letu na kutengeza timu nzuri ya taifa.


Lakini je vilabu vyetu vya Simba na Yanga vinapigania wachezaji kutoka kwenda kucheza Ulaya?


Sababu mara nyingi tumekua tukiona hivi kwa matakwa yao binafsi vikiwanyima fursa wachezaji wao kujiunga na vilabu vikubwa, lakini endapo wangetambua umuhimu wa wachezaji hawa kwenda vilabu vikubwa basi vilabu vyetu vingekua vikipigana kuwapeleka wachezaji wao kufanya majaribio mara kwa mara kama vilabu vya Afrika Magharibi nchi kama Nigeria, Ghana na Senegal kucha kutwa wanapeleka wachezaji wao nchi za Ufaransa, Italia, Ubeligiji na Uholanzi kufanya majaribio katika vilabu mbalimbali kwa gharama zao.


Hivyo basi watanzania tusisherekee tu Mbwana Samatta kwenda Ulaya bali tumtumie kama daraja la kupitia wachezaji wengine.


0655995405

LIVERPOOL YAIGALAGAZA MANCHESTER UNITED

 Liverpool manager Jurgen Klopp punches the air with delight after Firmino's strike doubled their first-leg advantage
Liverpool vijogoo vya Anfield  wameanza vyema kampeni zao kwenye michuano ya Europa League hatua ya 16 bora baada ya kuiangushia kipigo Manchester United cha bao 2-0 kwenye uwanja wa Anfeild jana usiku.
 Liverpool fans show their passion for their club ahead of kick-off in their Europa League first-leg encounter
Ulikuwa usiku mzuri kwa mashabiki wa Liverpool usiku wa jana na kuwa mchungu kwa Mashabiki wa Manchester United waliosafiri kuja kuiangalia timu yao wakizani wataendeleza ubabe wao kwa Liverpool lakini haikuwa hivyo.
 Firmino (right) fired home Liverpool's second goal during the Europa League first leg encounter with this left-footed strike
  Goli la pili lililoimaliza Manchester United usiku wa jana likifungwa na Firmino.
.....
Kikosi cha Jurgen Klopp kilitawala mchezo huo kwa asilimia kubwa ya mchezo huo wa kwanza kati ya timu hizo za Premier League giants huku kocha huyo wa kijerumani akifurahia ushindi wake dhidi ya United.


Daniel Sturridge aliipa Liverpool goli la kuongoza dakika ya 15 kwa mkwaju wa penati baada ya Memphis Depay kumfanyia madhambi Nathaniel Clyne kwenye eneo la hatari penati ambayo imezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wadau wakikosoa kwamba ilikuwa ni nje ya penalty box.

Liver vs Man U 1
Roberto Firmino akaongeza bao jingine kwa shuti kali la karibu zikiwa zimesalia dakika 17 pekee mchezo huo kumalizika.


United haikutengeneza hata nafasi moja ya kufunga, ubora wa golikipa wao David de Gea  ndiyo umeikoa United kuchezea idadi kubwa ya magoli kwenye mchezo huo baada ya mlinda mlango huyo wa Hispania kuokoa michomo mingi.

Rekodi zilizowekwa kwenye mchezo huo:
Liver vs Man U 2
  • Manchester United hawajashinda mchezo wowote wa ugenini kati ya michezo yao sita iliyopita kwenye hatua ya moano ya michuano ya Ulaya, wamepoteza michezo mitano kati ya hiyo. 
  • United imepata clean sheet moja kwenye mechi 10 walizocheza kwenye uwanja wa Anfield kwenye mechi za mashindano yote.
  • Daniel Sturridge amefunga magoli matano na ku-assist goli moja kwenye mechi saba dhidi ya United kwenye mashindano yote.
  • United wamepigiwa mashuti nane on target dhidi ya Liverpool, mashuti mengi zaidi kuziuwa na klabu hiyo ndani ya mechi moja msimu huu.
  • Roberto Firmino amefunga magoli matatu mfululizo kwa mara ya kwanza kwenye mechi za Liverpool.

DIDA WA TIMES FM AELEZA KISA CHA KUTUKANWA NA MKE MDOGO WA MZEE YUSUPHU

Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amefunguka na kuzungumzia sababu ya kutukanwa katika mtandao wa kijamii na mke mdogo wa Mzee Yussuf, Chiku.
Mzee Yussuf Jumanne hii aliamua kuwaondoa wake zake wawili Leyla Rashid na Chiku katika mtandao wa Instagram baada ya kuwa wanatupiana maneno machafu kupitia mtandao huo hali ambayo inadaiwa ilikuwa inamchafua mume wao.

Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Dida amedai alitukanwa na Chiku ambaye ni mke mdogo wa Mzee Yussuf kwa madai alikuwa anampendelea mke mkubwa wa Mzee Yussuf, Leyla Rashid.

“Kusema ukweli kila mtu anajua jinsi wake zake Mzee Yussuf, Leyla Rashid na Chiku pamoja na wifi yao walivyokuwa wanarushiana matusi. Lakini mimi kama mimi niliwaHi kuzungumza na Chiku na baadaYe Leyla, lakini nilianza Chiku. Kila mmoja alikuwa anaeleza tatizo nini na kwanini wamekuwa wakitukanana katika mitandao ya kijamii, hawaoni kama wanamuaibisha mume wao! Basi kila mmoja akawa anazungumza kwa pande wake, siku nimezungumza na Leyla akazungumza mambo mengi sana, sasa Chiku baada ya kusikia akawa ananitukana mimi kupitia mitandao,” amesema Dida.

“Mimi binafsi sikumjibu vibaya nikawa namuelewesha nini maana ya uke wenza lakini akawa anaendelea kunitukana. Nikasema Mzee Yussuf ndiye anaweza kumaliza tofauti zao, ngoja nimtafute ili nizungumze naye, akakubali lakini siku ambayo aliniambia nitaongea naye akaniambia amepata dharura na pia hawezi kuja na kuzungumzia mgogoro wa familia yake kwani ataumaliza mwenyewe,” alisema Diva.

Bongo5 ilijaribu kumtafuta Mzee Yussuf ili kuzungumzia suala hilo kwakuwa linamshushia heshima yake, lakini alikataa na kusema tayari ameshafunga ukurasa wa kuzungumzia masuala ya wake zake kwenye vyombo vya habari.

Pia Mzee Yussuf alidai tayari ameshawakataza wake zake kutumia mtandao wa Instagram kwa kuwa ndio chanzo cha ugomvi wao huku na yeye akijipanga kuondoka katika matumizi ya mtandao huo.

Hata hivyo Bongo5 haikuishia hapo, ilizungumza na mtu wa karibu wa Mzee Yussuf ambaye hakutaka kutajwa jina lake na kueleza jinsi mgogoro huo unavyomuumiza kichwa Mzee Yussuf.

“Kweli amewaambia hakuna mtu kutumia mitandao wa Instagram na atakayetumia kwa siri ndiyo talaka yake. Unajua haya mambo huwezi kujua nani ni mkorofi kwa sababu unashangaa tu mambo yamezuka na huwezi kuelewa chanzo chake ni nini. Lakini hii hali inamuumiza sana Mzee kusema kweli, sema watu wa nje wanamchukulia poa,” alisema.

Chanzo:Bongo5

ANGALIA PICHA KALI ZA WACHEZAJI WA AZAM FC WAKIWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWL.JULIUS NYERERE(JNIA) KUELEKEA AFRIKA KUSINI


12795538_1135961929777495_5973066540374643315_n
Wachezaji wa timu ya Azam FC hivi sasa wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA), tayari kabisa kwa safari ya kuelekea jijini Johannesburg Afrika Kusini saa 4 asubuhi leo kucheza mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bidvest Wits ya huko.


Mchezo huo utafanyika Jumamosi ijayo (Machi 12) katika Uwanja wa Bidvest kuanzia saa 1.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na kikosi hicho kimeondoka na morali kubwa kabisa ya kupata matokea mazuri ugenini baada ya kufanya maandalizi ya kutosha.
10392501_1135964079777280_6697366497168637111_n 12376795_1135963526444002_362414547287540873_n 12718138_1135962129777475_630214351908762530_n 12791078_1135965076443847_5516784093513636450_n 12794499_1135963303110691_6885570628233574923_n 12794550_1135968233110198_7139524904883754227_n 12795538_1135961929777495_5973066540374643315_n 12801474_1135966103110411_6621679224069370764_n 12802980_1135968139776874_6571324300157269958_n 12804746_1135965529777135_5359882632666947344_n 12804893_1135962249777463_8835464798289719902_n 12809535_1135966663110355_4149863084798262334_n 12814665_1135967313110290_1751571246852653353_n


MZEE YUSUPHU AFUNGUKA BAADA YA WAKE ZAKE KUCHAMBANA INSTAGRAM

WAKATI wanawake duniani kote leo wakiadhimisha siku ya wanawake duniani, wake wa mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusufu, Leila Rashid na Chiku wamekatazwa kutumia tena mtandao wa Instagram.

Wanawake hao wamekatazwa kutumia mtandao huo na endapo watatumia kwa siri mume wao huyo amewaeleza kwamba ndiyo itakuwa talaka yao.

Mzee Yusufu amechukua uamuzi huo baada ya hivi karibuni kuzuka kwa majibizano ya wake zake hao kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsap na Instagram.

Akizungumza kwenye mahojiano na kipindi cha taarabu kinachorushwa na Redio Clouds, Mzee Yusufu, alisema mtandao huo ndio chanzo kikubwa cha kukuza mgogoro huo.

“Nimewatoa wake zangu wote kwenye mtandao huu ambao ndio nimeona umekuza sana mgogoro huu na mimi pia nipo njiani kutoka katika akaunti hiyo ili ibaki kwa ajili ya kazi tu na endapo nitagundua yeyote ana simu ya siri ambayo anaitumia kuingia kwenye mtandao huo ndiyo itakuwa talaka yake.

“Hivi tunavyozungumza wake zangu wote hawana akaunti za Instagram, zinazoendelea kusambaza maneno ni majina feki na ndiyo nimeshaamua hivyo,” alisema.

Mtanzania

Wasanii Waidai Mamilioni Ya Pesa IKULU....Deni hilo Liliachwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Ikulu imeahidi kufanyia kazi madai ya Chama cha Wasanii Wachoraji Tanzania (Chawata), ambayo waliyawasilisha jana, kikilalamikia ofisi hiyo katika awamu ya nne iliyokuwa chini ya Rais Jakaya Kikwete, kuwacheleweshea malipo yao ya Sh. milioni 53.6.

Kwa mujibu wa taarifa ya Chawata kwa vyombo vya habari jana, fedha hizo zimetokana na kazi za sanaa ambazo zilichukuliwa na serikali ya awamu ya nne kutoka kwa wafanyabiashara wa eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam na kupelekwa Ikulu.

Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, alithibitisha kuwapo na madai hayo na kusema kuwa yatafanyiwa kazi ndani ya wiki moja kuanzia jana.

“Ni kweli Ikulu inadaiwa, lakini ni deni la awamu ya nne, kwa hiyo tumewaomba kuwakamilishia madai yao ndani ya wiki moja, baada ya kufanya uhakiki ili kujiridhisha,” alisema Msigwa.

Awali, Katibu wa Chawata, Cuthbert Semgoja alisema waliahidiwa kulipwa fedha hizo kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana lakini hadi sasa hawajalipwa.

"Tuliuza kazi zetu Ikulu kwa makubaliano ya kulipwa baadaye tangu Agosti mwaka jana, hadi leo hii (jana) bado hatujaweza kupatiwa pesa zetu," alisema na kuongeza:

“Mchakato wa kazi zetu ulianza mwishoni mwa mwezi wa nane kwa kamati husika, kupitia katika maeneo ya wasanii, ili kuweza kufanya chaguzi ya sanaa wanazohitaji. Walijiridhisha kwa kuchukua baadhi ya sanaa kutoka kwa wanakikundi kwa ahadi ya kufanya malipo mara moja kabla ya uchaguzi mkuu lakini hadi sasa bado malipo hayo,” alisema Semgoja.

Alisema baada ya chama kuona muda wa malipo unakwisha, walichukua jukumu la kupiga simu kwa mhusika ambaye walikuwa wakifanya naye biashara hiyo kwa niaba ya Ikulu, lakini jibu lake lilikuwa `malipo yenu yanaandaliwa.'

“Baada ya mwezi mmoja kufanya biashara hiyo, tulianza kumpigia simu mtu mmoja ambaye ndiye alikuwa anahusika na sisi tangu mwanzo wa biashara yetu hadi mwisho, lakini majibu tunayopewa ni kusubiri tu, tumechoka sasa,” alisema.

Alisema mawasiliano waliyokuwa wanafanya na mtu kutoka Ikulu ambaye alijitambulisha (jina tunalo), ndiye aliyekuwa akiwapa majibu hayo kuhusu madai yao.

Aliongeza kuwa kulingana na ahadi waliyopewa kulipwa kabla ya uchaguzi mkuu na mlolongo wa ahadi zinazojirudia, walianza kufanya mawasiliano wao kwa wao ili  kufahamu nini kinachoendelea kuhusu malipo yao na kugundua kuwa kuna tatizo.

“Ilifika hatua simu zetu hazipokelewi, kila tunapopiga mhusika hapokei simu zetu, ndipo hapo tulipohisi kuna mchezo unaendelea kati ya mtu huyo na chama chetu,” alisema.
© Copyright Udaku Kijiweni
Back To Top